MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU
HUDUMA YA USHINDI KATIKA NENO - TANZANIA
MJUA MUNGU WA KWELI
Katika Yoh 17:1-3 tunaona Bwana wetu Yesu aliomba maombi haya akisema, UZIMA WA MILELE NDIO HUU WAKUJUE WEWE, MUNGU WA PEKEE, NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA.Wakristo ndiyo watakubaliana na mimi kwa mujibu wa biblia lakini tungekuwa tuna soma kitabu cha kiislam kingesomeka hivi WAKUJUE WEWE MUNGU WA PEKEE NA MUHAMAD ULIYEMTUMA. Nikiwa na maana Mungu tunaemwamini ni huyo huyo mmoja kama ndivyo, lakini mambo hayako hivyo wako miungu wengi mchana wa leo. Baba yangu mmoja wa Kiroho akaandika hivi " kumbe kuna miungu wengi katika uso wa dunia. Biblia imesema kuwa wengine mungu wao ni TUMBO, wengine mungu wao ni mungu wa dunia hii, yaani SHETANI.
Mtanzania mwenzangu kama Mungu wako ni huyu tunayesema ni wa pekee kwa mujibu wa Imani ya wakristo wote na waislamu wote na mambo yako hivi tunavyochukiana; basi naweza kusema siyo sisi Watanzania tunagombana bali ni shetani anatutumia; haiwezekani wala haingii akilini kuwa watanzania wanauwana kwa sababu zifuatazo za kawaida mno ambazo hazina nafasi katika ulimwengu wa mtu na uhai;
2)MUUNGANO. Nataka tujiulize swali moja kama ugomvi wetu ni juu ya Muungano ambao wako wengine wanautaka na wengine hawautaki je swala la kuuwawa kwa padre,wachungaji ama shehe,kutekwa kumwagiwa tindikali waandishi wa habari linakujaje hapo?
Viongozi wa dini,ama madhehebu hamna aliyemtuma mtu kufanya hili na kama amekutuma ukakubali basi wewe ndiye kafiri ama pepo. Jamani Tanzania imeingiliwa na kitu kinachoitwa nguvu na mipango ya kuzimu hapa tunahitaji Wakristo kuomba na Waislamu kuomba pia ili Mungu huyu tunayemsema ni mmoja tuweze kumuona. Watanzania wanathamini dini kuliko mtu, wanathamini dhehebu kuliko mtu, wanathamini kabila kuliko mtu hivi dunia ni ya thamani kiasi gani zaidi ya mtu biblia takatifu inasema hivi
Marko 8:36 kwa kuwa itamfaidia nini mtu aupate ulimwengu wote apoteze nafsi yake"Ndugu msomaji neno linasema hata upate dunia yote haiwezi kufika thamani ya mtu mmoja sasa ninyi mnaouwa watu kwa ajili ya matakwa yanu binafsi mnafikiri mna mbingu yenu
Hivi karibuni mfuasi kijana wa Ukomunisti alimwandikia mchumba wake barua ya kuvunja uchumba, baada ya kufunguliwa kutoka gerezani. Aliandika hivi:
"Sisi Wakomunisti tunakufa sana. Sisi ndiyo hupigwa risasi au kunyongwa au kudhihakiwa au kufukuzwa kazi na kufanyiwa maudhi mengi tu ili maisha yetu yasiwe mazuri. Asilimia fulani yetu huuawa au kufungwa. Tunaishi katika umaskini kabisa. Kila senti tunayopata ambayo ni zaidi ya mahitaji tuliyo nayo tunatakiwa kuitoa kwa chama. Sisi Wakomunisti hatuna muda wala fedha kwa ajili ya kwenda sinema sana, au kwenye matamasha ya muziki, au kula nyama, au kukaa nyumba nzuri, au magari mapya. Tunaitwa waliobobea. Sisi tumebobea katika ukomunisti. Maisha yetu yanatawaliwa na jambo moja kubwa: Kuufanya ulimwengu mzima kuwa wa Kikomunisti. Sisi tuna mtazamo katika maisha ambao hakuna kiasi chochote cha fedha kinachoweza kuununua. Tuna jambo tunalopigania, tuna kusudi dhahiri maishani mwetu. Tunaweka makusudi yetu na nia zetu kwenye nafasi ya pili maana nafasi ya kwanza ni kuteka ulimwengu. Basi, japo maisha yetu binafsi yanaonekana kuwa magumu au ubinafsi wetu unaonekana kuteseka kwa sababu ya kujiweka nafasi ya pili chini ya chama, tunafidiwa sana kwa wazo kwamba kila mmoja wetu kwa njia yake ndogo tu anachangia kuleta kitu kipya na cha kweli na kilicho bora kwa ajili ya mwanadamu.
Kuna kitu kimoja tu ambacho nina shauku nacho sana maishani, nacho ni Ukomunisti. Ni maisha yangu, ndiyo biashara yangu, ndiyo dini yangu, ndiyo kazi yangu, ndiyo mpenzi wangu, ndiyo mke wangu, ndiyo pumzi yangu na chakula changu. Ninautumikia mchana na kuota juu yake usiku. Ukomunisti umenishika sana, na nguvu yake inazidi badala ya kupungua kadiri muda unavyopita. Basi, siwezi kuingia kwenye urafiki, wala kujiingiza kwenye mapenzi wala mazungumzo bila ya kuvihusisha hivyo na hiki kitu changu ambacho ndicho kinasukuma maisha yangu na kuyapa nguvu. Ninawatazama watu, vitabu, hoja na matendo kulingana na jinsi vyote hivyo vinavyoathiri Ukomunisti, na jinsi wao wanavyoutazama. Tayari nimekwisha fungwa kwa ajili ya msimamo wangu, na kama ni lazima, niko tayari kupigwa risasi kwa ajili hiyo hiyo."
Kuna mengi ya kujifunza hapa ;
Moja Ingawa amedanganywa bado anaamini kuwa yuko sahihi mbele za Mungu na dunia nzima
Pili anaamini kwa kufanya hivi ndiyo anapata Baraka ama thawabu kwa Mungu
Tatu anataka kwenda mbinguni baada ya maisha ya hapa duniani, wanadamu wote wanachogombana kwenye imani ni kuhusu mbinguni ila nashangaa wanaouwa wakifikiri ndiyo suluhisho nafikiri tumelogwa;
Maana Yesu Kristo anasema toeni pepo,fufueni wafu na wala siyo toeni waislamu kwa sababu wao ni mapepo;hamna mahali tunaruhusiwa kuuwa,kutesa
Na Mtume Muhamad anasema toeni makafiri ambayo ndiyo mapepo na kuwapa mahitaji wenye shida yaani wanaokufa na njaa yaani wafufueni na sio toeni Wakristo ndiyo makafiri ; Hii ndiyo maana halisi ya Viongozi waliotutangulia ama waliotoka kwa Mungu; lakini leo hatupendani hata kidogo embu mtazame mtanzania ujione wewe mwenyewe kwa nini kujiuwa unauwa Mtanzania mwenzako yaani ni kama kumuua mama yako au baba yako. Fikiria una muua mzazi wa mwingine ama mme wa mwingine ama mke weka kwa sababu ya siasa au muungano hii siyo sawa ni pepo. Naamuru lishndwe juu ya Tanzania yetu lirudi lilikotoka.
2)KUCHINJA; Ngojeni niseme kwa kweli kuwa uyaone kwa nini watu tumekosa utu namna hii kwani akichinja mwislam au mkristo kosa liko wapi, unajua kabla hujaleta hoja zako za kujidai unayo dini lazima uwaze hivi je ingekuwa tunapumua kwa kutumia dini ni nani angepumua vizuri kuliko mwenzake ukipata jibu wewe ndiye unayestahili kuchinja. Nitakalo kusema ni hili wakristo wanao muongozo wao wa IMANI na Waislam pia kwa wakristo wanaruhusiwa kuchinja na kuuza na kula pia waislam nao sasa kusema nani asile aliyechinja nani ni kumkosoa Mungu aliyetuumba ili tupokee vitu vyote kwa shukrani.
Ikiwa unaweza kumtengeneza mnyama wako unalo la kujisifu lakini wanyama tumewakuta hata kabla hajaumbwa mwanadamu hawa wanyama wapo na Mungu aliyewaweka kwa ajili ya kitoweo kwa wote; Hii ni kufuru yaani ni kucheza na Baraka na Mungu aweza pia kuwaondoa wote;Lililokuu hapa tunapaswa kumshukuru Mungu kwa sababu wapo walio na ujuzi katika kuchinja vitoweo hivi na wanajipatia ajira; Kwangu mimi sivyo achinje mkristo awe mwislam hainipunguzii wala kuniongezea kwa maana najua tena nahakikisha miungu si kitu ila Mungu ni mmoja aliyeziumba mbingu nan chi maana kwake siudhurishwi kwa chakula 1kor 8:4-8; Wito wangu kwa Wakristo tumuombe Mungu ili jambo hili lipate ufafanuzi mzuri ili pande zote zielewe; nafikiri limekaa kiajira zaidi maana haliitaji shule kwa hiyo wale ambao hawana ajira ndiyo wanagombana nani apate ajira pale, maana tunapochinja tunalipwa kulingana na mnyama kwa hiyo halipo kiimani zaidi; bali kimaslahi maana kama ungekuwa unafanya kama ibada yaani kuchinja bila malipo wewe umekuwa mwema kiasi gani hata ujitolee bure, tupo hapo kimaslahi. Nafikiri ili jambo kama litaachiwa watu wa imani Fulani ili wafanye,basi nashauri wafanye kama wito bure bila kulipwe chochote maana hamna kitu cha imani chenye kulipwa.
3) DINI; tutaangalia tatizo la dini ambalo linachangiwa na upepo wa kiaarabu kwa maana ya kuwa huu ni ugomvi ambao haumuhusu Mtanzania yoyote wale wanaojiingiza wanafuata mkumbo tuu ugomvi huu ulianza tangu Ishmael na Isaka kwa neon ama ahadi ya Mungu pia na Yakobo pamoja na Esau tena hawa walianza kugombana tangu tumboni mwa mama yao lakini mimi na wewe ni watanzania ambao hata kibiblia hatuna neon linalotutaja isipokuwa kwa imani mbona tunataka kujifanya kama sisi tuliyo matawi yaliyopandikizwa kwenye mzabibu usiyo wa asili tunajifanya tumebeba shina badala ya shina kubeba tawi?.ile, Warumi 11:17-20
Dini ni kama wanyama wabebao mzigo au walimao ardhi ni wajuzi wa kubeba lakini hawali walichobeba na wala kwa wakati wao ni kwa huruma za aliyewatuma wanakula na dini ndivyo si chombo cha kukupeleka mbinguni bali ni chombo cha kukujulisha ama kukonyesha njia na namna ya kuishi ili kufika pale sasa utakubaliana na mimi kama unafanya vurugu kwa masilihi ya dini hiyo siyo bali ni biashara ni zao la chakula na mkulima ni unayemwamini.
MJUA MUNGU WA
KWELI
Yoh 17:1-3 tunaona Bwana wetu Yesu aliomba maombi haya akisema, UZIMA WA MILELE NDIO HUU WAKUJUE WEWE, MUNGU WA PEKEE, NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA. Biblia imesema kuwa wengine mungu wao ni TUMBO, wengine mungu wao ni mungu wa dunia hii, yaani SHETANI. 2kor 4:4 inasema hivi hatulichanganyi neno la Mungu na uwongo ila wanaochanganya ni wale wanaomtumikia mungu wa dunia hii yaani dogo mimi namwitaga shetani dogo, kwa sababu halingani hata na kidole cha Mungu. Nimekuletea msitari huu ili uweze kujua hata leo wengi Mungu wao ni tumbo ni pesa. Kwa matukio yanayojiri utangundua hili ngoja nikufikirishe kidogo wakristo wengi wanaamini matukio ya Zanzibar ya kuuwawa Padre ama Mchungaji ni waislamu ndiyo wanaohusika lakini utakuwa umekosea maana aliye mwislamu wa kweli hawezi fanya hivyo na kama ni wao watakuwa wameenda mbali sana na maneno wanayosema kuwa ni dini ya haki tena ya mnyazi mungu. Wanaoua na kuendeleza chuki ni wahuni na watu wenye vikundi vya siri kama wachawi ni sawa na wanaowakata alubino mikono siyo wacha Mungu hao wanamtumikia shetani. Unajua kama mtu ni Mkristo alafu akaenda kwa mganga akaambiwa akaoge baharini na kesho akaendelea kujiita ni Mkristo hapo anajidanganya si Mkristo soma 1Yohana 2:4 tunasoma hivi ikiwa tunasema tunamfuata Yesu alafu tukaenda gizani twajidanganya kweli haimo kwetu. Bali anatumia mwavuli huo tu kwa hiyo kwa wakristo wa kweli jambo hili hatuitaji kutumia kisasi kujiridhisha huko ni kutumia silaha ya adui kupigana sisi silaha yetu ni maombi na upendo geuza hasira kwa Upendo Rum 12:19;Huku ukijuwa ya kwamba wakristo wakweli huwa hawana ushabiki wa dini ama madhehebu. Kuna kikundi kinaitwa uamsho chenye mwavuli wa dini kwanza asante kwa Serikali kuwadhiti hawa siyo watu wa dini bali ni kikundi cha siri chenye kuwajumlisha na wasiyo na elimu ya Kimungu wanaingia bila kujua; Ninavyoelewa neno Yamsho yaani ni kutokutumia akili za kawaida,wala mabavu,wala silaha na hata maandamano bali ni kutumia nguvu ya maombi na dua kusababisha mambo kuwa sawa na unavyotaka.

Mfano mzuri kwa Wakristo tunaupata kwa Yesu Kristo na mitume wake walikuwa wanaenda sehemu majangwani wakifunga na kuomba kwa ajili ya mambo wanayotaka yatokee,
Na waislam tunajuwa Mtume Muhamad alipoona mambo hayaendi anavyotaka alienda mbali majangwani na akakaa kweenye pango kule unafikiri alienda kufanya nini kama si kufanya dua na mungu alisikia dua yake akampa mwongozo ambao ni kuruani, hata sisi tunaweza kufanya hivyo badala ya vurugu za nani achinje,nani avunje muungano nani ni nani acheni kutumika ninyi watu ombeni mtapata majibu ya kila kitu na ikimpendeza mungu wenu atawapeni vitabu vingine vitakafujo kama hivi vitakatifu mmshindwa kuvielewa na kuviamini
deomassawe@gmail.com na 0655 216 729. USHINDI kwa UPENDO
deomassawe@gmail.com na 0655 216 729. USHINDI kwa UPENDO
No comments:
Post a Comment